Let's Talk..Mental health App
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Let's Talk..Mental health App, Dar es Salaam.
💚 Let’sTalk – Mental Health
🧠 Tunasaidia kufungua mazungumzo ya afya ya akili
🤝 Jukwaa la support, therapy & community
✨ Pakua app yetu & anza safari yako ya uponyaji, Anxiety,Depression, na mengine yanayo husu afya ya akili
10/10/2026
🧠 **HERI YA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI 2026** 🌍💚
Leo, tarehe **10 Oktoba 2026**, tunaungana na dunia nzima kuadhimisha Siku ya Afya ya Akili Duniani.
K**a **Mwanasaikolojia Tiba (Clinical Psychologist)**, napenda kuwakumbusha kuwa afya ya akili ni sehemu muhimu ya afya na ustawi wa kila mmoja wetu.
💚 **Kusikiliza ni upendo. Kuelewa ni msaada. Na kutafuta huduma ya kitaalamu ni hatua ya ujasiri.**
Tusimhukumu mtu kwa changamoto anazopitia. Badala yake, tumpe nafasi ya kuzungumza, tumsikilize kwa huruma na tumsaidie kupata msaada unaofaa.
🧠 *“Kusikiliza na kushirikikisha watu wenye changamoto za afya ya akili katika kuleta mabadiliko.”*
Afya ya akili ni jukumu letu sote. Tujenge jamii yenye uelewa, huruma, matumaini na isiyo na unyanyapaa.
**Kumbuka: Huhitaji kupitia changamoto zako peke yako. Kuomba msaada ni hatua ya nguvu, si udhaifu.** 💚
**, Tanzania 🇹🇿
26/09/2026
Some days, surviving is the bravest thing you can do.
Follow this page upate elimu,msaada,juu ya afya yako ya akili..
14/09/2026
Septemba ni mwezi maalumu wa kuongeza uelewa kuhusu kuzuia vifo vya kutoa/kukatisha uhai. Mambo kadhaa ningependa kuyaandika katika kuyafikiri.
1. Mbali na takwimu za Shirika la Afya Duniani zinazosema zaidi ya watu laki saba duniani kila mwaka hukatisha maisha yao. Ni wakati wa kuangalia zaidi ya hizi takwimu.
2. Vifo vingi vya kukatisha uhai huwa vipo viashiria kadha wa kadha ambavyo mtu anayefikiria hadi kutekeleza tukio la kujitoa uhai huonesha. Je, sisi k**a jamii huwa tunajali viashiria hivyo?
3. Mbali na kuwa vifo vya kujitoa uhai huhusishwa moja kwa moja na changamoto za afya ya akili au uwepo wa ugonjwa wa akili ( sonona ikiwemo) huchangia mtu kufikia hiyo hatua.
4. Watu wanaweza kusema, "Sioni haja ya kuishi", "Nimechoka kuishi", "nimepoteza thamani yangu". Kauli k**a hizi zinapojitokeza sisi jamii tunabebaje au kutoa msaada wa haraka?
5. Vipo visa vingine huripotiwa hata na vyombo vya habari kuwa mtu huyu kabla ya kutekeleza kujitoa uhai, ndugu wanasema, "Tulimwona ni mtu aliyekata tamaa", "mtu mwenye mawazo sana". Huenda viashiria hivi ni kengele muhimu ilohitaji jamii iwe daraja la msaada.
6. Jaribio moja la kujitoa uhai linatoa hatari zaidi ya majaribio mengine hapo baadae. Viashiria vyovyote vya hatari ni vyema mtu kupata msaada haraka wa kisaikolojia na pengine matibabu/msaada endapo nyuma ya jaribio hilo kuna changamoto ya afya ya akili au ugonjwa wa akili
7. Mtu kufikia ngazi ya kufikiria kujitoa uhai ni njia pekee ni wazi zipo pia sababu za kijamii na kisaikolojia zenye nguvu nyuma ya majaribio haya. Ni vyema tujenge nafasi ya msaada pale watu wapitiapo hali ngumu au kukutwa na jambo linalotikisa maisha yao kwa wakati huo kijamii, kiuchumi au kisaikolojia
8. Simu moja ya kujuliana hali yaweza kuokoa mtu mmoja ambaye wakati huo hujihisi kutengwa au upweke. Upweke pekee ni moja ya mazingira hatari yanayochochea fikra za watu kujiumiza au hata kujitoa uhai. Kundi kubwa hususani la wazee huwa na idadi kubwa ya visa vya kujitoa uhai na upweke ( loneliness) ikiwemo ya mazingira hatarishi kwao.
9. Tunaweza kuepusha vifo vya kutoa uhai kwa kushirikiana na jamii yote kwa kuanza, "kujali", "kuwaelewa watu wapitiapo vipindi vigumu", "kutohukumu bali kusikiliza zaidi na kutoa msaada".
10. Kuongeza mazungumzo ya jamii ikiwemo nafasi ya wazee, vijana, watoto kuhusu thamani ya maisha na namna ya kukabiliana na nyakati ngumu inaweza kuzuia visa vingi vya kujitoa uhai. "Community based mental health initiatives" ni muhimu sana. Rejea nzuri ni namna Friendship bench nchini Zimbabwe
Follow this page kwa taarifa,elimu na uelewa juu ya afya ya akili
14/09/2026
Ni nini kinachokusaidia kujisikia vizuri unapopitia siku mbaya sana kiakili?
10/09/2026
Siku ya Kuzuia Kujiua Duniani inatukumbusha kwamba uelewa, huruma na msaada unaotolewa kwa wakati vinaweza kuokoa maisha. Tuwe tayari kusikiliza, kuzungumza kwa uwazi kuhusu suala hili, na kuhamasisha watu kutafuta msaada wanapouhitaji.
'stalk mental health
07/05/2026
25/04/2026
KUTOJIAMINI KIMYA KINACHOUMIZA NDANI YA MTU 😔
Kutojiamini sio tu kusema “sijiamini”…
Ni sauti ya ndani inayokuambia: “Wewe hauwezi… haujatosha…”
Watu wengi wanapitia hali hii kimya kimya, huku nje wakionekana sawa kabisa.
💔 Dalili za kutojiamini:
• Kujiona huna thamani au hustahili vitu vizuri
• Kuogopa kujaribu vitu vipya kwa hofu ya kushindwa
• Kujilinganisha sana na wengine
• Kuomba ridhaa ya watu kila mara (people pleasing)
• Kushindwa kusema “hapana” hata pale inapobidi
🧩 Chanzo kinaweza kuwa:
• Maneno ya kuumiza kutoka utotoni au kwa watu wa karibu
• Kushindwa au kukataliwa mara kwa mara
• Mlinganisho wa maisha (hasa kupitia mitandao ya kijamii)
• Kukosa uthibitisho (validation) kutoka kwa watu muhimu
⚠️ Athari zake:
• Unapoteza fursa nyingi kwa sababu unaogopa
• Unaweza kuingia kwenye mahusiano yasiyo sahihi
• Unaweza kuishi maisha ya kujificha, sio ya kweli
🌱 Namna ya kuanza kujijenga upya:
✔️ Anza kujizungumza vizuri (positive self-talk)
✔️ Acha kujilinganisha kila mtu ana safari yake
✔️ Weka mipaka (boundaries) kwenye mahusiano
✔️ Fanya vitu vidogo vinavyokujengea ujasiri taratibu
✔️ Tafuta msaada k**a hali imezidi (rafiki au mtaalamu)
🤍 Kumbuka:
Kujiamini sio kuzaliwa nako ni kitu unachojenga kidogo kidogo kila siku.
✨ Usijidharau wewe ni muhimu kuliko unavyofikiria
Usikubali sauti ya ndani ikushushe thamani yako jifunze Kujikubali.
19/04/2026
🌿 JE, UNAJITAMBUA AU UNAISHI TU?
Watu wengi wanaishi maisha kila siku wanaamka, wanaenda kazini, wanarudi, wanacheka na watu… lakini ndani yao hawajijui kabisa.
Unajua nini kinachokuumiza?
Unajua nini kinachokufurahisha kweli?
Unajua kwa nini unachoka haraka kiakili au kihisia?
💭 Ukweli ni huu:
Bila kujitambua, unaweza kuishi maisha ambayo si yako.
Unaweza kujikuta unafanya vitu ili kufurahisha watu wengine, huku wewe mwenyewe ukipotea.
✨ Dalili kuwa hujajitambua vya kutosha:
• Unabadilika kulingana na watu unaokutana nao
• Unashindwa kusema “hapana” hata pale unapoumizwa
• Mara nyingi hujui unachotaka maishani
• Unajilaumu sana bila sababu
💡 Anza hapa kujitambua:
• Jitengee muda wa kukaa na nafsi yako (hata dakika 10 tu)
• Jiulize: “Ninajisikiaje leo, na kwa nini?”
• Andika mawazo yako (journaling)
• Kubali hisia zako usizikimbie
❤️ Kujitambua ni hatua ya kwanza ya kujipenda.
Na kujipenda si ubinafsi ni afya ya akili.
💬 COMMENT:
Leo umejifunza nini kuhusu nafsi yako?
👉 Follow page kwa maudhui zaidi ya afya ya akili kila siku.
19/04/2026
🌱 KUJILINGANISHA NA WENGINE NDIO MWIZI WA FURAHA YAKO 🌱
Kila siku tunaona maisha ya watu kwenye mitandao:
📸 Picha nzuri
💼 Mafanikio
💑 Mahusiano yanayoonekana kamili
Na taratibu tunaanza kujiuliza:
“Mbona mimi sipo hivyo?”
Ukweli ni huu:
👉 Unajilinganisha na highlight za maisha ya mtu, sio uhalisia wake
👉 Kila mtu ana safari yake, muda wake, na mapambano yake
👉 Usipojilinda, utaanza kujiona huna thamani bure
💡 Jifunze:
✔️ Kushukuru kidogo ulichonacho
✔️ Kuangalia maendeleo yako, sio ya wengine
✔️ Kujikubali ulivyo huku ukijiboresha
❤️ Wewe ni wa kipekee. Safari yako ni yako. Usiiharakishe kwa kuangalia wengine.
18/04/2026
💭 WAKATI MWINGINE SI UVIVU… NI KUCHOKA KIHISIA
Kuna siku unaamka lakini huna nguvu
Sio kwa sababu huwezi…
Bali moyo umechoka 💔
Unaahirisha mambo
Unakosa hamasa
Unajiona k**a huna maana
Lakini ukweli ni huu:
Hujavunjika unahitaji kupumzika.
🧠 Akili nayo huchoka k**a mwili
Na inahitaji:
✔ Mapumziko
✔ Mazungumzo
✔ Upendo
🌿 Jipe ruhusa ya kupumzika bila kujilaumu
🌿 Jipe muda wa kujirudisha polepole
💬 Usijilazimishe kuwa sawa kila siku wewe ni binadamu, sio mashine.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
000000
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Let's Talk..Mental health App posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.